Killa atakae kuokoka: zaidi ya yote imemlazimu kuishika Imani Katholiko.
Nayo asipoilinda pasipo kuipunguza wala kuiharibu: bila shaka atapotea milele.
Na Imani Katholiko ni hii: tumwabudu Mungu minoja katika Utatu, na Utatu katika Umoja;
Tusizichanganye nafsi: wala kuigawanya asili.
Kwa maana nafsi ya Baba mbali, nafsi ya Mwana mbali: nafsi ya Koho Mtakatifu mbali.
Bali Uungu wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu ni Uungu umoja: Uttikufu wao sawa, Ukuu wao wa milele.
Kama alivyo Baba, ndivyo alivyo Mwana: ndivyo alivyo Roho Mtakatifu.
Baba hakuumbwa, Mwana hakuumbwa: Roho Mtakatifu hakuumbwa.
Baba hana mpaka, Mwana hana mpaka: Roho Mtakatifu hana mpaka.
Baba wa milele, Mwana wa milele: Roho Mtakatifu wa niilele.
Walakini hakuna watatu walio wa milele: illa Mmoja aliye wa milele.
Kadhalika hakuna wata'tu wasioumbwa, wala watatu wasio na mpaka: illa mmoja tu asiyeumbwa, na mmoja tu asiye na mpaka.
Kadhalika Babani Mwenyiezi, Mwana ni Mwenyiezi: na Roho Mtakatifu ni Mwenyiezi.
Bali hakuna Watatu walio Wenyiezi: illa aliye Mwenyiezi ni mmoja tu.
Yivyo hivyo Baba ni Mungu, na Mwana ni Mungu: na Roho Mtakatif u ni Mungu.
Bali hakuna Miunguwatatu: illa Mungu mmoja tu.
Vivyo bivyo Baba ni Bwana, na Mwana ni Bwana: na Roho Mtakatifu ni Bwana.
Bali hakima Bwanawatatu: illa Bwana mmoja tu.
Kwa maana kama tunavyoshurutishwa kwa kanuni ya kweli ya Kikristo: kukiri ya kuwa killa nafsi ni Mungu na Bwana;
Kadbalika tunagombezwa na Imani Katholiko: tusiseme ya kuwa wako Miungu watatu au Bwana watatu.
Baba hakuumbwa na aliye yote: wala hakukhulukiwa wala hakuzaliwa.
Mwana anatoka katika Baba tu: bakuumbwa, wala hakukhulukiwa, bali anazaliwa.
Roho Mtakatifu anatoka katika Baba na katika Mwana: hakuumbwa,wala hakukhulukiwa, wala hakuzaliwa, bali anatoka.
Bassi yupo Baba mmoja tu, si Baba watatu; yupo Mwana mmoja tu, si Wana watatu: yupo Roho Mtakatifu mmoja tu, si Roho Watakatifu watatu.
Na katika Utatu huu hapana aliye wa kwanza na aliye wa baadae: hapana aliye mkuu zaidi na aliye mdogo.
Bali nafsi zote tatu ni wa milele: wa sawa wote.
Bassi katika mambo yote kama tulivyokwisha kusema: imetulazimu kuuabudu Umoja katika Utatu, na Utatu katika Umoja.
Bassi yeye atakae kuokoka: audhanie hivi Utatu.
Na zaidi ya haya, apate wokofu: imemlazimu kukuamini kwa moyo Kufanyika mwili kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Na Imani kamili ndiyo hii: tuamini, tukiri ya kuwa Bwaiia wetu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ni Mungu na Mwana Adamu.
Ni Mungu, ana asili ya Baba, amezaliwa kabla ya zamani zote: ni Mwana Adamu, ana asili ya Mama wake, alizaliwa katika zamani.
Mungu kamili na Mwana Adamu kamili: ana roho yenye akili na mwili wa Mwana Adamu.
Yu sawa na Baba kwa kuwa ni Mungu: Yu chini ya Baba kwa kuwa ni Mwana Adamu.
Na ijapokuwa yu Mungu na Mwana Adamu: yeye si wawili illa Kristo mmoja.
Yeye ni mmoja, si kana kwamba Uungu urnebadilika uwe mwili: bali kwa kuitwaa asili ya Mwana Adamu na kuiunga na Uungu.
Mmoja kabisa; si kwa kuzichanganya asili zile mbili: bali kwa kuwa Nafsi mmoja tu.
Kwa maana karaa roho yenye akili pamoja na mwili huwa Mwana Adamu mmoja: kadhalika Mungu na Mwana Adamu pamoja ni Kristo mmoja;
Aliyeteswa kwa wokofu wetu: akashuka mahali pa wafu, akafufuka siku ya tatu.
Akapaa mbinguni, anaketi mkono wa kuume wa Mungu Baba Mwenyiezi: kutoka huko atakuja kuwahukumu watu wahayi na wafu.
Atakapokuja yeye, wana Adamu wote watafufuka na miili yao: watatoa khabari za matendo yao.
Nao waliotenda mema wataingia katika uzima wa milele: nao waliotenda mabaya katika moto wa milele.
Hii ndiyo Imani Katholiko: killa mtu asiyeikubali kwa moyo hawezi kuokoka.
Utukufu una Baba, na Mwana: na Koho Mtakatifu;
Ulivyokuwa mwanzo: ulivyo sasa, utakavyokuwa milele. Amin.