Covenant Protestant Reformed Church
Bookmark and Share

Roho Ikaayo Kama Hua Wakati Wa Ubatizo Wa Yesu

Rev. Angus Stewart

 

Karibu majuma sita baada ya kumbatiza Bwana Yesu Kristo pale Mto Yordani, ushuhuda wa Yohana Mbatizaji kuhusu tukio hilo muhimu lilikuwa na hii kauli: "Niliona Roho ikaayo kama hua ikishuka na ikakaa juu yake" (Yohana 1:32). Wahubiri wote wanne wanaongea kuhusu Roho Mtakatifu kumshukia Masihi wakati wa ubatizo wake "kama hua" (Mathayo 3:16; Marko 1:10; Luka 3:22; Yohana 1:32). Kwa nini hua?

Kwanza hua ni ndege. Mungu alichagua kama ishara ya roho wakati wa ubatizo wa Yesu, si mnyama atembeaye juu ya nchi au samaki aogoleaye katika bahari bali ni ndege hurukaye angani (Mwanzo 1:20). Hoja ni rahisi kushika. Roho wa mungu aishiye mbinguni; ndege huruka juu yetu mbinguni. Roho wa Mungu aliwakilishwa na ndege wa anga, alitoa mwito wa kibingu kwa daraka na alimvisha Yesu na karama za kiungu katika ubinadamu wa Yesu kwa ajili ya kazi yake ya umma kama Masihi. Yohana Mbatizaji, katika ushuhuda kumhusu Kristo akibatizwa, alitangaza kuwa roho kama hua, ambaye ni ndege, "alishuka" (Yohana 1:32, 33) kutoka mbinguni (32).

Pili, Mungu alichagua hua kama ishara ya Roho wakati wa ubatizo wa Yesu kwa kuwa hua ni mpole na asiye na hatia (siye kama kunguru). Katika kauli ambayo imekuwa mithali, Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa lazima wawe "wapole kama hua" (Mathayo 10:16), kwa kuwa yeye alikuwa "mtakatifu asiyeuumiza, bila unajisi, anayetengwa kando na watenda dhambi" (Waebrania 7:26). Kwa nguvu ya roho kama hua, Bwana Yesu aliyekuwa mwenye hawezi kuumiza, asiye na hatia, safi na mtakatifu katika ubinadamu wake na kwa madaraka yake kama Mwokozi wetu. Hapa twaona umoja wa ishara ya hua na sauti kutoka mbinguni wakati Kristo anabatizwa: "Huyu ni mwanangu nimpendaye, ninayependezwa kwake" (Mathayo 3:17; Marko 1:11; Luka 3:22). Mungu hupendezwa mno na mwanawe maana haumizi na haana hatia kama hua.

Tatu, Mungu alichagua hua kama ishara ya Roho wakati wa ubatizo wa Yesu kwa maana hua hupendeza, hupendwa na hupenda (siye kama tumbusi). Hapa mtu hufikiria taswira ya hua hasa katika kitabu cha Wimbo Ulio Bora kinachowatambua kama waroro, na wenye manyoya na macho marembo, na wenye upendo na wenye uaminifu kwa wenzao (kwa mfano, Wimbo ilio Bora 1:15; 2:14; 4:1; 5:2, 12; 6:9). Hua wa kupendeza, mwenye upendo na wa kupendwa kutoka mbinguni na sauti ya Mungu kutoka mbingu husema hasa lilo hilo jambo: "Huyu ni mwanangu ninayempenda."

Nne, Roho Mtakatifu kwa mfano wa hua kutoka mbinguni hakumshukia Yesu akibatizwa bali pia alibakia kwa Yesu. Hii ilistajaabisha Yohana Mbatizaji, aliyetangaza kuwa roho kama hua "alikaa kwake" (Yohana 1:32) na kubakia juu yake (33). Funzo ni kuwa Roho humwita na humvisha Masihi kwa ajili ya huduma yake ya uuma, kwa kumwekelea ubinadamu wake karama za kiungu na neema kama asiyeuumiza na mwana wa Mungu apendezaye, akiwa na Roho akaaye kwake, Kristo alianza kuhubiri na kutenda miujiza, yote ambayo hakufanya kabla abatizwe- kuwekwa kama Nabii Mkuu wa Mungu au Kuhani au mfalme.

Kumbuka pia, mara ngapi na umuhimu wa "kubakia" na "Kukaa" katika Injili ya Yohana. Inaongea kuhusu ushirikiano wa kibinafsi  unaodumu na wa ndani. Mungu katika utatu, kwa roho yake kama hua, hukaa katika ushirikiano wa ndani, wa kudumu, wa kibinafsi, na wa kiagano pamoja na mwanawe asiyeuumiza na anayependwa. Si hili ni la kuvutia mno!

Tano, Mungu alichagua hua kama ishara ya roho katika ubatizo wa Yesu kwa maana, katika Bibilia, hua, juu ya yote, ni ndege za dhabihu (Mwanzo 15:9; Walawi 1:14-17; 5:7-10; 12:6-8; 14:22, 30-31; 15:14-15, 29-30; Luka 2:24; Yohana 2:14, 16). Ni rahisi kuona kwa nini hua wasiouumiza na wasio na hatia walichaguliwa na Mungu kama dhabihu, kuonyesha mapema ondoleo la dhambi.

Katika kuungana na ushuhuda wake kuwa roho kama hua alimshukia Kristo kutoka mbinguni (Yohana 1:32). Yohana Mbatizaji alitangaza: Tazameni mwana-kondoo wa Mungu, aondoleaye dhambi ya dunia" (29). Roho, katika hali ya hua wa dhabihu, alimwita na kumvisha Masihi mpendwa na asiyeuumiza ili awe mwana-kondoo wa dhabihu aliyebeba adhabu yetu iliyotupasa kulingana na makosa yetu.

Sita, Mungu alichagua hua kama ishara ya Roho wakati wa ubatizo wa Yesu Kristo kwa maana, hua, mwema kushinda ndege ye yote, ni ishara ya dunia. Pale kuumbwa vitu kwanza, "Roho wa Mungu alitembea(alitambaa au aliruka kama ndege) juu ya uso wa maji" (Mwanzo 1:2). Wakati wa gharika, hua asiyeumiza na anayependeza alitumwa kutoka safina mara tatu na hakurudi mara ya tatu (Mwanzo 8:8-12)! Ujumbe ni wazi: hasira ya Mungu imepita; dunia mpya hungojea! Huu ndio ushurikiano kati hua na kiumbe kipya.

"Dunia" (Yohana 1:29) aliyomfilia mwana-kondoo wa Mungu ni "Dunia" ya waaminio, ambao dhambi zao Kristo alizilipia na ambao Kristo huwaombea kama mtetezi (Yohana 3:16; I Yohana 2:1-2). Sio "dunia" aliyohukumu Mungu msalabani na asyoiombea Bwana Yesu (Yohana 12:31; 17:9).

Kwa kuwa mwana-kondoo wa Mungu alizifilia "dhambi za dunia" (Yohana 1:29), akikomboa watu wake "kutoka kila jamii, lugha, umati na taifa" (Ufunuo 5:9), kiumbe kikali pia "atafunguliwa kutokana na uharibifu" (Warumi 8:21). Maana binadamu  ni kichwa cha viumbe, binadamu alipoanguka, viumbe vilianguka na yeye. Kwa ukombozi na kufanywa upya kwa binadamu katika Kristo, dunia imekombolewa na itafanywa upya kama mbingu na dunia mpya. Roho, kama hua wa kupendeza na asiyeumiza, alimshukia na kukaa juu ya Bwana Yesu akibatizwa ili, kupitia dhabihu ya mwana-kondoo wa Mungu, kiumbe kipya kitakuja—dunia yenye urembo mtukufu na yenye usalama mno ambapo simba na mwana-kondoo watalala pamoja (Isaya 11:6-8; 65:25).